Gavana wa kaunti ya Kisii Simba Arati amedai wapinzani wake wamepanga njama ya kumuua kwa kumtilia sumu baada ya kushindwa kumbandua afisini.
Arati amesema njama hiyo inatokana na hatua yake ya kuziba mianya ya ufisadi iliyokuwa imekolea katika kaunti hiyo kabla ya kuingia afisini.
Alitoa matamshi hayo ya kushangaza Jumatano usiku katika shule ya msingi ya Nyabisia eneo binge la Bobasi akihudhuria hafla moja iliyoandaliwa na mwakilishi wodi ya Masuga Mashariki.
Gavana huyo aliongeza kuwa njama ya kumuua imetokana na kufeli kwa jaribio la kumng’atua mamlakani kufuatia hatua ya wawakilishi wengi wa wodi kupinga hoja hiyo.
Kumekuwa na msukosuko katika uongozi wa Arati hususan mwaka huu.