Bingwa wa zamani wa Afrika katika shindano la matembezi amefuzu kushiriki michezo ya Olimpiki ya jijini Paris Ufaransa .
Gathimba ambaye alikosa kushiriki makala ya mwaka 2020 ya olimpiki alifuzu kwa mashindano ya mwaka huu, baada ya kumaliza wa nne katika mashindano ya Dunia yaliyoandaliwa Budapest mwaka uliopita nchini Hungary.
Gathimba alisajili muda wa saa 1 dakika 18 na sekune 34 mwaka jana nchini Budapest.
Ni mara ya kwanza kwa mwanariaha huyo kufuzu kushiriki michezo ya Olimpikiki.
Fainali ya kilomita 20 matembezi katika michezo ya Olimpiki itaandaliwa Agosti mosi mwaka huu, ambayo pia itakuwa siku ya kwanza ya fani ya Riadha.