Home Kaunti Gari la Gavana wa Bomet lahusika katika ajali

Gari la Gavana wa Bomet lahusika katika ajali

0

Gari la Gavana wa kaunti ya Bomet, lilihusika katika ajali ya barabarani Jumatatu asubuhi katika eneo la Kipsarwet Bomet Mashariki.

Hata hivyo Gavana huyo na waliokuwa katika gari hilo hawakujeruhiwa, baada ya gari hilo kugongana na pikipiki, karibu na hoteli ya Fairhils.

Inasemekana mwwndeshaji wa pilkipiki hiyo alijaribu kuvuka barabara, ajali hiyo ilipotokea.

Kamanda wa polisi wa Bomet ya kati Musa Omar Imamai, alisema mwwndeshaji huyo wa bodaboda alipata majeraha na anapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Longisa.

Gavana Barchok, alikuwa akielekea afisini mwake ajali hiyo ilipotokea.

Website | + posts