Home Michezo Gambia yatinga kipute cha AFCON kwa mara ya pili

Gambia yatinga kipute cha AFCON kwa mara ya pili

Mataifa 22 yamejikatia tiketi kwa fainali hizo zitakazoandaliwa kati ya Januari 13 na Februari 11 mwaka ujao nchini Ivory Coast .

0

Timu ya taifa ya Gambia ilijikatia tiketi kwa makala ya 34 ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika mapema mwaka ujao nchini Ivory Coast, baada ya kutoka nyuma na kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Congo katika mchuano wa kundi G uliosakatwa ugani Stade De Marrakech nchini Morocco.

Gambia almaarufu The Scorpions walimaliza katika nafasi ya pili kundini G nyuma ya Mali wakizoa alama 10.

Wachezaji wa Gambia wakisherehekea kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2024 uwanjani Marrakech

Timu zilizowahi tiketi ni Nigeria,Guinea Bissau,Burkina Faso,Cape Verde,Senegal, Msumbiji,Afrika Kusini,Morocco,Tunisia,Equitorial Guinea,DR Congo na Mauritania.

Mataifa mengine yaliyofuzu ni Zambia,Ivory Coast,Mali,Gambia,Algeria,Tanzania,Ghana,Angola,Misri na Guinea.

Nafasi mbili za mwisho zilizosalia zitajazwa Jumanne wakati wa mechi ya kundi C mjini Yaunde kati ya wenyeji Cameroon dhidi ya Burundi.

Namibia waliokalimisha mechi zao wanaongoza kundi hilo kwa alama 5 ,moja zaidi ya Cameroon na Burundi wanaoshikilia nafasi ya pili.