Home Habari Kuu Gachagua: Wanawake, vijana na walemavu wapewe zabuni

Gachagua: Wanawake, vijana na walemavu wapewe zabuni

Gachagua alisema maafisa wakatili wa ununuzi wamewapiga kumbo makundi hayo dhidi ya kufanya biashara na serikali.

0

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa maafisa wa ununuzi kuwapa kipaunbele wanawake, vijana na walemavu katika utoaji wa zabuni.

Gachagua alisema maafisa wakatili wa ununuzi wamewapiga kumbo makundi hayo dhidi ya kufanya biashara na serikali.

Akihutubia kongamano la pili kuhusu mchakato wa ununuzi na usambazaji katika kaunti ya Mombasa, Gachagua alisema makundi hayo ya watu yanapaswa kupigwa jeki Kwa mujibu wa sheria, sera na sheria zingine zilizopo kuhusu ununuzi.

Naibu huyo wa Rais alisema wanawake, vijana na wanaoishi na ulemavu, hawaja nufaika inavyostahili kutokana na maafisa wakatili ambao hushirikiana na wasambazaji bidhaa kuwafungia nje wale wanaistahili kunufaika.

“Baadhi ya watu husajili kampuni kwa kuwatumia wanawake, lakini wanawake hao hawapo. Vijana wanasajiliwa kama wafanyabiashara, lakini wanaofanya biashara hiyo sio vijana, sawia na wanaoishi na ulemavu. Nawasihi ( Maafisa wa ununuzi) kuwaruhusu makundi haya ya watu kufanya biashara,” alisema Gachagua

Aidha Gachagua alidokeza kuwa wale wanaostahili kufanya biashara na serikali wanajulikana, lakini kutokana na mchakato haramu, wanawake, vijana na walemavu wanafungiwa nje.

“Tunatoa wito wa maadili katika mchakato wa ununuzi na utoaji zabuni. Lazima tufuate mchakato mzima. Wale ambao hawawezi kufanya kazi jinsi inavyohitajika, lazima wakabiliwe na sheria,” alidokeza Gachagua.