Home Kimataifa Gachagua: Uhusiano kati yangu na Rais Ruto ni thabiti

Gachagua: Uhusiano kati yangu na Rais Ruto ni thabiti

0
kra
Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa hakikisho kwamba uhusiano kati yake na Rais William Ruto ni thabiti. 
Gachagua amewaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kueneza taarifa za uongo juu ya uhusiano kati yake na Rais Ruto.
“Hakuna uhasama kati yangu na Rais Ruto. Tuna uhusiano mzuri na kama msaidizi wake mkuu, yeye hutafuta ushauri kutoka kwangu kuhusu masuala mbalimbali, kwa mfano kubuniwa kwa serikali ya muungano kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho. Amenipa majukumu mengine mbalimbali kama vile kuongoza na kuratibu uhusiano kati ya serikali kuu na serikali za kaunti ikiwa ni pamoja na kuongoza Baraza la Bajeti na Kiuchumi kati ya Serikali (IBEC),” alisema Gachagua jana Jumapili usiku wakati akihojiwa na vyombo vya habari vinavyotangaza katika lugha ya mama kutoka eneo la Mlima Kenya.
“Mimi ni msaidizi mkuu wa Rais na sikinzani na msimamo wake. Wajibu wangu ni kuwahudumia Wakenya na kutekeleza majukumu niliokabidhiwa na Rais. Kuhusiana na kubuniwa kwa serikali ya muungano, nilimuunga mkono. Mawaziri wapya wateule wakiwemo wale walioteuliwa kutoka upinzani wanakaribishwa ili tuisongeshe nchi mbele pamoja.”
Matamshi yake ynakuja huku kukiwa na uvumi kuwa uhusiano kati yake na Rais Ruto kuzorota umesuasua katika siku za hivi karibuni.
Kiini cha uvumi huo ni kukosa kwa Gachagua kuhudhuria baadhi ya mikutano muhimu ya serikai nyakati zingine.
Isitoshe, wakati Rais Ruto akitangaza kufutiliwa mbali kwa Mswada wa Fedha 2024 kutoka Ikulu ya Nairobi, Gachagua hakuwepo.
Badala yake, aliandaa mkutano na wanahabari kutoka mjini Mombasa na kuhutubia taifa kutoka huko katika hatua ambayo ilikoselewa na baadhi ya waangalizi wa masuala ya kisiasa.
kra