Home Habari Kuu Gachagua: Tunajiandaa vilivyo kukabiliana na athari za El Nino

Gachagua: Tunajiandaa vilivyo kukabiliana na athari za El Nino

0

Serikali za kaunti na washirika wa kimaendeleo, watakutana na maafisa wa serikali kuu, kuangazia rasilimali zinazohitajika kukabiliana na athari za mvua ya El Nino.

Akizungumza katika kaunti ya Isiolo, naibu huyo wa Rais alisema mkutano huo utaimarisha mikakati inayowekwa kuhakikisha maisha hayatapotea kutokana na mvua hiyo.

Siku ya Alhamisi, Gachagua aliandaa mkutano mwingine na wadau kukadiria hali ilivyo katika kukabiliana na athari za mvua ya El Nino.

“Nimeandaa mkutano siku ya Jumanne wiki ijayo, kujadili rasilimali zilizotengwa na serikali ya kitaifa, zile za kaunti na washirika wa kimaendeleo,” alisema Gachagua.

Gachagua aliyasema hayo wakati wa ibada ya shukrani ya Katibu katika idara ya mafuta Mohamed Liban.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa, imesema mvua ya El Nino itaanza mwezi Oktoba mwaka huu na kuendelea hadi mwezi Januari mwakani.

Website | + posts