Home Habari Kuu Gachagua: Serikali itasitisha zimwi la ujangili Kerio Valley

Gachagua: Serikali itasitisha zimwi la ujangili Kerio Valley

0

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema serikali itasitisha ujangili Katika eneo la Kerio Valley, akisema haitakubalika tena kwa watu kupoteza maisha mikononi mwa majangili.

Naibu huyo wa Rais alisema serikali ya Kenya Kwanza itatimiza ahadi ilizotoa kwa wakazi wa eneo hilo, ya kukabiliana na zimwi la ujangili kikamilifu.

Akizungumza siku ya Ijumaa mjini Iten alikozindua miradi ya uhamasisho katika eneo bunge la Keiyo Kaskazini, Gachagua alisema serikali itahakikisha janga hilo linasitishwa katika eneo hilo.

“Tuliahidi kumaliza wizi wa mifugo katika eneo la bonde la Kerio. Hii ndio serikali itasitisha uovu huo. Kwa sasa wizi huo umekabiliwa, na utakabiliwa milele,” alisema naibu huyo wa Rais.

Gachagua alisema kuwa maafisa wa usalama waliopelekwa katika eneo hilo kudumisha amani na usalama, watasalia katika eneo hilo hadi pale ujangili utaangamizwa kabisa.

“Maafisa wa usalama watasalia katika eneo hili hadi amani itakapo patikana. Watu wetu hawatauawa kiholela tena na majangili serikali ikiwa mamlakani,” aliongeza Gachagua.

Naibu huyo wa Rais alisema miradi  iliyonyimwa ufadhili kutokana siasa mbovu katika eneo la North Rift ikiwemo mabwawa ya Arror, Kimwarer dams na uwanja wa  Kimariny, itakamilishwa kwa wakati ili iwanufaishe wananchi.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here