Home Biashara Gachagua: Mchakato wa kuifanyia mabadiliko sekta ya kahawa utachukua muda

Gachagua: Mchakato wa kuifanyia mabadiliko sekta ya kahawa utachukua muda

0
Naibu Rais Rigathi Gachagua wakati akikutana na wakulima wa Baricho
Naibu Rais Rigathi Gachagua wakati akikutana na wakulima wa Baricho

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema mchakato wa kuifanyia mabadiliko sekta ya kahawa nchini utachukua muda mrefu na sasa anatoa wito kwa wakulima wa zao hilo kuwa na subira. 

Alisema hayo alipokutana na wakulima ambao ni wanachama wa Chama cha Ushirika cha Kahawa cha Baricho leo Jumatatu asubuhi.

“Wakulima wa Baricho walielezea imani yao katika utawala wa Rais William Ruto katika kuzitatua kabisa changamoto zinazoikumba sekta hiyo. Wanaelewa kwamba mchakato wa kuifanyia sekta hiyo mabadiliko utachukua muda na utakuwa wenye machungu tele; lakini watakuwa na subira,” alisema Gachagua.

Anasema aliwataarifu hatua iliyopigwa katika kuifanyia sekta ya kahawa mabadiliko, ikiwa ni pamoja na ziara yake nchini Colombia alikofanya mazungumzo ya ngazi za juu na wanaoweza kununua zao hilo humu nchini.

Gachagua ameahidi kuwa utawala wa Kenya Kwanza utaifanyia sekta ya kahawa mabadiliko makubwa kwa manufaa ya wakulima ambao kwa muda mwingi wamepunjwa na mawakala.

 

Website | + posts