Home Kimataifa Gachagua: Marekebisho katika sekta ya kahawa yanazaa matunda

Gachagua: Marekebisho katika sekta ya kahawa yanazaa matunda

Naibu wa Rais alisema zao la kahawa limevutia bei iliyoimarika katika soko la kahawa la Nairobi, kutokana na marekebisho yaliyoanzishwa mwaka jana.

0
Naibu Rais Rigathi Gachagua, katika maonyesho ya kimataifa ya kilimo ya Nairobi.

Naibu Rais Rais Rigathi Gachagua, amesema marekebisho yanayotekelezwa katka sekta ndogo ya kahawa yanazaa matunda, akidokeza kuwa wakulima wamenufaika pakubwa kutokana na bei iliyoimarika.

Akizungumza leo Jumatano alipofungua rasmi maonyesho ya kimataifa ya kilimo ya Nairobi katika uwanja wa Jamuhuri, naibu huyo wa Rais alisema zao la kahawa limevutia bei iliyoimarika katika soko la kahawa la Nairobi, kutokana na marekebisho yaliyoanzishwa mwaka jana.

“Marekebisho Katika sekta ndogo ya kahawa, yamezaa matunda, huku minada 47 ikiandaliwa tangu mwezi Agosti mwaka 2023 hadi leo. Bei ya mfuko wa kilo 50 wa kahawa, imeongezeka hadi dola 237, kutoka dola 188 kabla ya marekebisho hayo,” alisema Gachagua.

Wakati huo huo Gachagua alisema vyama 15 ya ushirika sassa vinawasilisha kahawa katika soko la kahawa la Nairobi, ikilinganishwa na hapo awali ambapo chama kimoja kiliwasilisha.

Naibu huyo wa Rais alisema serikali imejitolea kuongeza fedha kwa hazina ya ustawi wa kahawa, inayosimamiwa na chama cha ushirika cha kahawa cha New Kenya Planters Cooperative Union.

“Katika mwaka wa kifedha wa 2024/25, tumetenga shilingi bilioni 3 kwa hazina ya ustawi wa kahawa,” alidokeza Gachagua.

Website | + posts