Home Biashara Gachagua: Hatutapumzika hadi tuifanyie mabadiliko sekta ya kahawa

Gachagua: Hatutapumzika hadi tuifanyie mabadiliko sekta ya kahawa

0

Juhudi za kuifanyia sekta ya kahawa mabadiliko kwa manufaa ya wakulima wa zao hilo zinaendelea vizuri. 

Naibu Rais Rigathi Gachagua ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mabadiliko hayo yanatimia, leo Alhamisi alifanya mkutano na Mawaziri Rebecca Miano wa Biashara na Simon Chelugui wa Vyama vya Ushirika na Maendeleo ya Biashara Ndogo na Kati kutafuta njia za kuiboresha sekta hiyo.

Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman pia alihudhuria mkutano huo uliofanyika katika makazi rasmi ya Naibu Rais mtaani Karen.

“Nilifanya majadiliano zaidi na Balozi wa Marekani nchini kenya Meg Whitman na timu yake kukubaliana juu ya njia na makataa ya kupata moja kwa moja soko la Marekani kwa ajili ya wakulima wetu wa kahawa,” alisema Gachagua baada ya mazungumzo hayo aliyoyataja kuwa yenye tija.

“Tunapiga hatua.”

 

Website | + posts