Home Habari Kuu Gachagua: Bara Afrika liondoe hitaji la viza

Gachagua: Bara Afrika liondoe hitaji la viza

Kulingana na Gachagua, teknolojia ni muhimu katika kufanikisha utangamano miongoni mwa raia wa Afrika.

0

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuondoa hitaji la viza, ili kutoa fursa kwa vijana kusafiri na kutangamana bila vikwazo barani humu.

Akizungumza siku ya Jumatatu wakati wa hafla ya kufunga kongamano la YouthConnekt Africa la mwaka 2023, lililoandaliwa katika jumba la mikutano ya Kimataifa, KICC jijini Nairobi,  Naibu Rais alisema vijana wana talanta tofauti na wanahitaji kupewa motisha ya kusafiri katika bara hili ili kukuza maendeleo.

Gachagua alisema kuwa Rais William Ruto anafanya juhudi kuhakikisha hitaji la viza linaondolewa barani Afrika, ili kuchochea ubadlishanaji wa mawazo, teknolojia na utamaduni miongoni mwa maswala mengine.

Kulingana na Gachagua, teknolojia ni muhimu katika kufanikisha utangamano miongoni mwa raia wa Afrika, akidokeza kuwa kongamano hilo liliafikia lengo la kuwaleta vijana pamoja.

“Tunaishi nyakati ambazo mipaka inakosa umuhimu. Teknolojia inatupatia fursa ya kushirikiana baina ya mataifa na mabara,” alisema Gachagua.

Alisema Rais Ruto ameonyesha jinsi kutokuwa na mipaka barani Afrika kunaweza unganisha bara hili.