Home Kimataifa Gachagua ashauriana na Balozi wa China Zhou Pingjian

Gachagua ashauriana na Balozi wa China Zhou Pingjian

Mkutano huo unajiri kabla ya ziara rasmi ya naibu huyo wa Rais katika Jamuhuri ya China.

0
Naibu Rais Rigathi gachagua, akutana na balozi wa China hapa nchini Zhou Pingjian.
kra

Naibu Rais Rigathi Gachagua leo Jumanne alikuwa mwenyeji wa Balozi wa China hapa nchini Zhou Pingjian katika makazi yake rasmi mtaani Karen.

Mkutano huo unajiri kabla ya ziara rasmi ya Naibu huyo wa Rais katika Jamhuri ya China.

kra

Wakati wa mkutano huo, Gachagua alidokeza kuwa ziara yake inalenga kuimarisha biashara baina ya mataifa hayo mawili, hususan katika bidhaa za kilimo ambako anatarajiwa kupigia debe kahawa, majani chai na maparachichi kutoka hapa nchini.

Maparachichi kutoka nchini Kenya ni miongoni mwa bidhaa ambazo huuzwa nchini China kwa wingi, tangu nchini hiyo ya Mashariki mwa bara Asia kutangaza kufungua soko lake kwa lengo la kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

“Tulijadiliana kuhusu maeneo yenye maslahi ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na kuimarisha bisahara na uwekezaji,” alisema Gachagua.

Mkutano huo unajiri miezi michache kabla ya China kuandaa kongamano la tisa kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) jijini Beijing huku Kenya ikitarajiwa kushiriki.

Website | + posts