Home Kimataifa Gachagua apongeza bunge la kaunti ya Nyandarua kwa kupitisha sheria ya vileo

Gachagua apongeza bunge la kaunti ya Nyandarua kwa kupitisha sheria ya vileo

0
kra

Naibu Rais Rigathi Gachagua amepongeza bunge la kaunti ya Nyandarua kwa kupitisha sheria ya kudhibiti vileo katika eneo hilo.

Akizungumza katika makazi yake rasmi huko Karen, Gachagua alisema bunge hilo limekuwa la kwanza kupitisha sheria hiyo na kwa kufanya hivyo limechagua kuokoa kizazi ambacho kingeangamia kwa amtumizi ya pombe.

kra

Gachagua alikuwa mwenyeji wa wawakilishi wadi wa kaunti Nyandarua ambao walimpokeza nakala ya sheria hiyo almaarufu “Nyandarua County Alcoholic Drinks Act, 2023”.

Naibu huyo wa Rais anashikilia kwamba ni lazima ushindi upatikane katika vita dhidi ya pombe haramu na mihadarati.

Alimpongeza pia Gavana wa kaunti hiyo Badilisha Kiarie, ambaye alitia saini sheria hiyo akisema alidhihirisha kujitolea kwake kuhudumia watu wa kaunti hiyo.

Sheria hiyo mpya imeafikiwa kupitia juhudi za viongozi wa serikali kuu na serikali ya kaunti ya Nyandarua na Naibu Rais amehimiza kaunti ambazo bado hazijapitisha sheria sawia kuiga mfano wa Nyandarua.

Gachagua aliwasilisha pia pongezi kutoka kwa Rais William Ruto kwa viongozi hao wa kaunti ya Nyandarua kwa kuitikia wito wa kuokoa vijana kutokana na pombe na mihadarati.

Website | + posts