Home Taifa Gachagua amwomba Ruto msamaha

Gachagua amwomba Ruto msamaha

0
Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua.
kra

Naibu Rais Rigathi Gachagua anayekabiliwa na masaibu na hatari ya kufurushwa ofisini amemwomba msamaha Rais William Ruto, siku mbili kabla ya kufika bungeni kujitetea.

Gachagua akihudhuria ibada katika afisi yake mtaani Karen siku ya Jumapili, amesema kuwa hajui makosa yake dhidi ya Ruto, ila akaomba msamaha endapo amemkosea Rais.

kra

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Gachagua kuonekana kulegeza msimamo mkali tangu hoja ya kumbandua ilipowasilishwa kwenye bunge la kitaifa mapema wiki iliyopita na mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse.

Hoja hiyo ilipata uungwaji mkono wa wabunge 291 wanaotaka Gachagua atimuliwe huku 58 pekee wakikosa kuusaini.

Kwa upande wake, Rais Ruto akihudhuria ibada alikwepa kuzungumzia swala hilo na badala yake kuzungumzia kuutupilia mbali mswada unaolenga kudhibiti makanisa nchini.

Mswada huo umeandaliwa na Seneta wa Tana River Danson Mungatana.

 

Website | + posts