Home Burudani Freddie Jackson kuongoza uhamasisho kuhusu maradhi ya figo

Freddie Jackson kuongoza uhamasisho kuhusu maradhi ya figo

0
kra

Mwanamuziki wa Marekani Freddie Jackson ambaye alivuma sana miaka ya 1980 ametangaza kwamba anaugua ugonjwa wa figo.

Kwenye video aliyochapisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram, Jackdon wa umri wa miaka 67 sasa alisema kwamba ameamua kuweka wazi hali yake ya kiafya baada ya kuwaza kwa muda.

kra

“Nimepatikana na ugonjwa wa figo. Safari yangu imekuwa yenye changamoto nyingi lakini nimeamua kuiendeleza kwa uwazi na uvumilivu.” alisema Jackson kwenye video hiyo.

Hatua ya kutangaza hali hiyo alisema inachochewa na haja ya kubadili ulimwengu na kutoa uhamasisho kuhusu maradhi ya figo.

Jackson alitangaza kwamba ameshirikiana na wakfu wa kitaifa wa figo nchini Marekani kutoa uhamasisho kuhusu ugonjwa huo huku wakisaidia walioathirika.

urther announced that he has partnered with the National Kidney Foundation to raise awareness about kidney health and provide support to those impacted by the condition.

Alishukuru mashabiki wake kwa kusimama naye akisema ameamua kutumia maisha yake kama jukwaa ya kuelewesha umma kuhusu maradhi ya figo ambayo huathiri wamarekani weusi kwa kiwango kikubwa.

Website | + posts