Home Kimataifa FOCAC 2024: Beijing yaahidi msaada zaidi kwa ajenda ya usalama wa chakula...

FOCAC 2024: Beijing yaahidi msaada zaidi kwa ajenda ya usalama wa chakula barani Afrika

0
Watafiti wa China na Kenya wanafanya kazi katika maabara ya pamoja ya Kenya-China ya biolojia katika Chuo Kikuu cha Egerton nchini Kenya. (Picha/Hisani)
kra

China imetangaza nia yake ya kuendelea kusaidia nchi za Afrika katika juhudi za kutokomeza uhaba wa chakula.

Wakati wa mkutano wa 2024 wa ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Beijing, maafisa wa ngazi ya juu wa China walisisitiza juhudi za serikali ya Rais Xi Jinping za kuyasaidia mataifa ya Afrika kutumia uwezo wa kilimo ili kuhakikisha usalama wa chakula.

kra

Wakiongozwa na Bw. Xu Jianping, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa idara ya ufunguzi wa mkoa wa kitengo cha maendeleo na mageuzi ya taifa (NDRC), maafisa hao walisisitiza kujitolea kwa China kutoa msaada wa kilimo kwa Afrika.

Bw. Xu alieleza kuwa China itaharakisha mikakati iliyothibitishwa ambayo ni pamoja na kugawana utaalamu wa kilimo na teknolojia na Afrika, pamoja na kukuza maendeleo ya mazao yanayostahimili hali ya hewa ili kuongeza tija ya kilimo.

“Kwa upande wa ushirikiano wa kilimo, China imefungua taasisi 45 katika nchi za Afrika, ambazo zinabadili maendeleo ya teknolojia ya kilimo na kuvutia nchi za Afrika,” alisema.

Zaidi ya hayo, Bw. Xu aliangazia jinsi ahadi ya China katika ushirikiano wa kilimo inavyowezeshwa kupitia jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na mpango wa ukanda mmoja na njia moja (BRI). Hii, alisema, imesababisha kuanzishwa kwa vituo vingi vya maonyesho ya teknolojia ya kilimo barani Afrika, kwa lengo maalum la kukuza kupitishwa kwa aina za mazao ya juu kulingana na hali ya hewa.

Aidha, alidokeza kuwa wataalam wa kilimo kutoka taifa la China kwa sasa wanafanya kazi katika nchi kadhaa za Afrika kuhamisha mbinu za juu za kilimo na aina za mbegu za hali ya juu kupitia utafiti wa kina, na kusababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula cha ndani.

Mfano mmoja mashuhuri katika ushirikiano huu ni maabara ya pamoja ya China na Kenya ya Biolojia, iliyoanzishwa kwa pamoja mnamo 2016 na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Nanjing cha China na Chuo Kikuu cha Egerton cha Kenya. Wanasayansi wa China wanashirikiana na wenzao wa Kenya kubuni aina za mazao yanayostahimili magonjwa na yenye kiwango cha juu, na hivyo kushughulikia ukosefu wa chakula barani Afrika.

Wanafunzi kutoka kanda zote za Afrika Mashariki na Kati wanajiandikisha katika taasisi hii ili kuongeza elimu yao kilimo.

Mpango mwingine uliofanikiwa ni ule wa Nigeria, ambapo wataalam wa China wametengeneza mbegu za mpunga zenye kiwango cha juu ambazo zimeongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mchele nchini humo. Mbegu hizo mpya zimepata umaarufu na sasa zimepandwa katika karibu theluthi mbili ya majimbo ya tafa hilo, na kuashiria maendeleo makubwa katika uzalishaji wa mchele wa taifa.

Kwa mujibu wa Bw. Xu, China itaendelea kutumia uwezo wake wa utafiti wa kilimo kusaidia miradi ya ndani inayoshughulikia ukosefu wa chakula, kuonyesha kujitolea kwa mazoea endelevu ya kilimo na kushirikiana na mataifa ya Afrika.

Xu alisema mkakati huo unaandamana na lengo la Beijing la kuimarisha usalama wake wa chakula huku ikizisaidia nchi za Afrika katika kukabiliana na changamoto za kilimo.

Kando na haya alitaja hatua ya China kuongeza kwa kiasi kikubwa uagizaji wake wa bidhaa za kilimo kutoka Afrika, ikiwa ni pamoja na parachichi, kahawa, mananasi, korosho, na mengineyo.

“Ushirikiano huu wa kibiashara unalenga kuagiza bidhaa maalum za Afrika na kuboresha uzalishaji wa kilimo kupitia mipango mbalimbali,” alisema.

Katika miaka ya hivi karibuni, anasema uagizaji wa maua, matunda na mboga kutoka Afrika umeongezeka, ukisaidiwa na utekelezaji wa sera ya kutoza ushuru kwa nchi nyingi za Afrika.

Majukwaa kama vile maonyesho ya kimataifa ya uagizaji wa China na maonyesho ya uchumi na biashara ya China na Afrika alivitaja kuwa maeneo muhimu katika kukuza bidhaa za kilimo za Afrika na kuongeza kujulikana kwao katika soko la China.

Alisema mipango hii, pamoja na juhudi zingine zitakazotangazwa katika mkutano wa FOCAC, zinaonyesha dhamira ya China ya ushirikiano wa kilimo na Afrika, kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa chakula, na maendeleo ya kiuchumi.

“China itaendelea kuimarisha ushirikiano wa miundombinu ya kiufundi na nchi za Afrika kwa pamoja na kuendesha miradi mikubwa ya kihistoria, kupanga na kukuza kundi jipya la miradi ya ushirikiano karibu na mahitaji yao ya kiuchumi na kijamii ya nchi za Afrika,” alisema.

Eric Biegon
+ posts