Home Burudani Filamu ya Bobi Wine yakosa kushinda tuzo ya Oscar

Filamu ya Bobi Wine yakosa kushinda tuzo ya Oscar

0

Filamu ya Bobi Wine: The People’s President imekosa kushinda tuzo ya Oscar katika kitengo cha filamu bora ya matukio halisi yaani “Best Documentary Film”.

Kazi hiyo ambayo iliandikwa, kutayarishwa na kuelekezwa na Moses Bwayo, Christopher Sharp na John Battsek iliwasilishwa kuwania tuzo hizo ambapo ilikuwa ikishindanishwa na “20 Days in Mariupol” ya Mstyslav Chernov, Raney Aronson-Rath na Michelle Mizner.

Nyingine ni “To Kill a Tiger” ya Nisha Pahuja, Cornelia Principe na David Oppenheim, “Four Daughters” ya Kaouther Ben Hania na Nadim Cheikhrouha pamoja na “The Eternal Memory” ya Maite Alberdi

Filamu ya “20 Days in Mariupol” ndiyo ilinyakua tuzo ya kitengo hicho na inahusu vita nchini Ukraine vilivyoanza baada ya wanajeshi wa Urusi kutekeleza uvamizi nchini humo.

Mwelekezi wa filamu hiyo Mstyslav Chernov ni mwanahabari wa Ukraine ambaye alinakili matukio ya uvamizi wa Russia nchini Ukraine hasa mjini Mariupol mwanzo wa mwaka 2022.

Kazi hiyo ilizinduliwa rasmi kwenye tamasha ya filamu ya Sundance mwaka 2023, ambapo ilipokelewa vizuri na walioitazama wengi wakiipigia uatu kuibuka na ushindi kwenye tuzo za Oscar awamu ya 96.

Matukio ya wakati huo Chernov anayataja kuwa kama vita vya tatu vya dunia hisia anazoshikilia hadi sasa.

Filamu hiyo ilishinda tuzo ya filamu bora ya matukio halisi kwenye tuzo za Bafta Uingereza na tuzo za chama cha waelekezi wa filamu nchini Marekani mwaka 2022.

Website | + posts