Home Kaunti Familia zilizoathiriwa na mashambulizi Lamu zapokea msaada

Familia zilizoathiriwa na mashambulizi Lamu zapokea msaada

0

Familia ambazo ziliathiriwa moja kwa moja na mashambulizi ya kigaidi katika Lokesheni ya Salama kaunti ya Lamu, zimepokea msaada kutoka kwa kanisa la African Inland Church – AIC.

Kati ya familia hizo, 12 zilizopoteza wapendwa wao na mali yao baada ya nyumba zao kuchomwa moto zimepokea bidhaa za nyumbani, makazi, chakula, pikipiki na vifaa vya kufanyia biashara.

Kulingana na baadhi ya waathiriwa, maisha yao yamekuwa magumu kwa sababu hawajakuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya kimsingi baada ya kupoteza kila kitu na wanaogopa kurejea kwenye mashamba yao kujijenga upya.

Mchungaji wa kanisa la AIC Mpeketoni Bernard Baya alisema kwamba msaada waliopokea watu hao utawasaidia kujikimu na kurejelea hali yao ya kawaida ya kiuchumi pole pole.

Website | + posts