Home Habari Kuu Familia ya marehemu Too yashinda kesi ya shamba

Familia ya marehemu Too yashinda kesi ya shamba

0

Familia ya mwanasiasa wa zamani wa chama cha KANU marehemu Mark Too, imeshinda ya umiliki wa kipande cha ardhi cha ekari 25,000 mjini Eldoret.

Hii inafuatia hatu ya makama ya upeo kuamua kuwa maskwota 3,00, waliokuwa wanadai umiliki wa shamba hilo hawana stakabadhi zinazohitajika kumiliki shamba hilo.

Kwenye uamuzi huo uliosainiwa na jaji mkuu Martha Koome, maskwota hao waliowakililishwa na kampuni ya Sirikwa Squaters Group, wamezuiliwa kuingia shambani humo.

Koome alitoa uamuzi huo Pamoja na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu ,majaji Mohamed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndungu, Isaac Lenaola na William Ouko.

Maskwota hao walikuwa wameshinda kesi zote katika mahakama ya chini ikiwemo mahakama ya rufaa.

Kesi hiyo ilianza mwaka 2012 wakati kampuni ya Sirikwa Squatters, iliposhtaki familia ya marehemu Too wakidai umiliki wa shamba hilo.

Website | + posts