Home Kaunti Familia ya Kiuna yataka kuomboleza faraghani

Familia ya Kiuna yataka kuomboleza faraghani

Askofu Kiuna alikuwa mwanzilishi mwenza wa kanisa la Christian Jubilee. Alifariki akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi.

0
Askofu Allan na Kathy Kiuna. Picha/Hisani.
kra

Familia ya marehemu Askofu Allan Kiuna aliyefariki Jumanne, imesema inataka kuomboleza kifo cha mpendwa wao faraghani.

Kupitia kwa taarifa kutoka kanisa la Jubilee Christian, familia hiyo imeelezea shukrani zake kwa wale waliowasiliana nao, huku ikisema ipewe fursa ya kuomboleza faraghani.

kra

“Ni kwa huzuni kubwa leo tunatangaza kifo cha mpendwa Askofu Allan Kiuna….kama kanisa na familia, tunatoa shukrani kwa wale wote waliotusaidia hususan kutoka kanisani. Tunaomba tupatiwe fursa kuomboleza faraghani, wakati huu mgumu,” ilisema taarifa hiyo.

Kanisa hilo lilimsifu Askofu huyo, likisema aliguza mioyo ya watu wengi na alikuwa na ari ya kuhudumu sio tu hapa nchini lakini pia Kimataifa.

“Imani yake na kujitolea kwake kuhudumu kanisani na katika jamii, kumeacha kumbukumbu kwa wale wote waliomjua. Hakuwa tu kiongozi wa kanisa, pia alikuwa baba, babu na rafiki,” iliongeza taarifa hiyo.

Askofu Kiuna alikuwa mwanzilishi mwenza wa kanisa la Christian Jubilee. Alifariki akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi.

Website | + posts