Home Habari Kuu Familia ya Kenyatta yaongoza hafla ya kuweka wakfu kanisa walilojenga

Familia ya Kenyatta yaongoza hafla ya kuweka wakfu kanisa walilojenga

0

Familia ya Rais wa kwanza wa nchi hii Jomo Kenyatta hususan mke wake Mama Ngina Kenyatta na mwanawe Uhuru Kenyatta ambaye pia alikuwa Rais wamekabidhi rasmi kanisa walilojenga kwa heshima ya hayati kwa uongozi wa kanisa Katoliki.

Hayo yalifanyika jana Jumamosi Disemba 16, 2023, huko Ichaweri katika kaunti ya Kiambu ambapo pia kanisa hilo liliwekwa wakfu kwa ajili ya kuendeleza injili.

Kanisa hilo la Mtakatifu Yohana Ichaweri, lilijengwa na Mama Ngina katika eneo ambalo awali Kenyatta alikuwa amejenga kanisa jingine mwaka 1971.

Mama Ngina alielezea kwamba Kenyatta alitaka kuwe na kanisa ambalo lingetumiwa na jamii ya eneo hilo, wazo alilorejea nalo kutoka kizuizini wakati huo.

Askofu wa jimbo la eneo la Nairobi la kanisa Katoliki Phillip Anyolo ndiye aliongoza misa ya jana akiwa ameandamana na viongozi wengine wa dini.

Rais wa zamani Uhuru Kenyatta alishukuru wote waliochangia kwa njia moja au nyingine ili kufanikisha ndoto ya mamake huku akimpongeza kwa kujitolea kuhakikisha inatimia.

Kanisa hilo ndilo la tisa sasa kati ya makisa ya Parokia ya Malaika Mkuu Gabrieli, Mutomo.

Website | + posts