Home Burudani Familia ya Aretha Franklin yaelekea mahakamani kwa sababu ya mali yake

Familia ya Aretha Franklin yaelekea mahakamani kwa sababu ya mali yake

0

Kesi ya urithi wa mali ya marehemu mwanamuziki Aretha Franklin ilianza jana Jumatatu katika mahakama moja huko Michigan. Kesi hiyo inahusisha watoto wake wa kiume watatu kutokana na hatua ya mama huyo ya kukosa kuacha wosia wa kuelekeza urithi wa mali yake.

Aretha aliaga dunia miaka mitano iliyopita akiwa na umri wa miaka 78 kutokana na maradhi ya saratani.

Mpwa wa Franklin aitwaye Sabrina Owens, ambaye alikuwa msimamizi wa mali yake wakati huo, anasema alipata nakala tofauti za wosia katika makazi ya Aretha huko Detroit.

Anasema nakala moja ilikuwa chini ya mto wa kochi na nyingine akaipata imefungiwa kwenye kabati.

Wanawe Franklin wamegawanyika kuhusu nakala hizo tofauti huku wawili wakitaka wosia wa mama yao wa tarehe 31 Machi, 2014 uchukuliwe kuwa halali huku mmoja akitaka wosia wa mwaka 2010 uchukuliwe kuwa halali.

Mmoja wa watoto wanne wa kiume wa marehemu Aretha Franklin aitwaye Clarence Franklin, ni mlemavu, amewekwa chini ya utunzi kisheria na hahusiki kwenye kesi hiyo.

Watoto hao wanataka mahakama itoe mwelekeo kuhusu jinsi watagawana mali ya marehemu mama yao inayojumuisha mapato endelevu ya muziki, pesa na mali nyingine.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here