Faith Odhiambo ndiye Rais mpya wa 51 wa chama cha mawakili nchini, LSK.
Hii ni baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzi wa chama hicho uliondaliwa kote nchini Alhamisi.
Odhiambo alitwaa wadhifa huo baada ya kuwashinda wagombea wengine wanne ambao ni Carolyne Kamende, Harriet Mboche, Peter Wanyama na Bernard Ngetich.
Alipata kura kura 3,113 akifuatwa kwa karibu na Peter Wanyama kwa kura 2,165.
Hadi kuchaguliwa kwake, Odhiambo amekuwa Naibu Rais wa LSK anayeondoka Eric Theuri ambaye muhula wake wa kuhudumu umekamilika.