Home Habari Kuu Ezra Chiloba asimamishwa kazi

Ezra Chiloba asimamishwa kazi

0

Ezra Chiloba amesimamishwa kazi kama mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchiniCAK.

Hatua ya kumsimamisha kazi ilitangazwa na Bi. Mary Mungai mwenyekiti wa bodi ya CAK.

Uamuzi wa kumsimamisha kazi Chiloba uliafikiwa katika kikao cha bodi Jumatatu, Septemba 18, 2023.

Bodi hiyo ilimteua Christopher Wambua kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa CAK.

Chiloba amehudumu katika wadhifa huo kwa muda wa miaka miwili. Alichukua mahala pa Francis Wangusi mwaka 2021.

Kabla ya kujiunga na mamlaka ya mawasiliano nchini, Chiloba alikuwa mkurugenzi mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini IEBC.

Website | + posts