Timu za Uingereza na Uholanzi zimefuzu kwa nusu fainali ya kipute cha bara Ulaya kinachoendelea nchini Ujerumani kutokana na ushindi dhidi ya Uswizi na Uturuki mtawalia.
Mechi ya Uingereza na Uswizi iliishia matuta ya 5-4 baada ya sare ya bao moja kwa moja katika muda wa kawaida na ule wa ziada.
Bao la Uswizi lilitingwa na Breel Embolo dakika ya 75 kisha Bukayo Saka akakomboa dakika tano baadae.
Kwenye robo fainali ya pili, Uturuki iliona lango kupitia Samet Akaydin dakika ya 35.
Stefan de Vrij alisawazisha dakika ya 70 kabla ya beki Mert Müldür kujifunga dakika ya 76 hivyo kuivusha Uholanzi.
Kufuatia ushindi huo, timu hizo zitamenyana tarehe 10 saa nne usiku.