Home Kimataifa Ethiopia ‘yazuia mashambulizi ya wanamgambo 450 wa Al-Shabaab’

Ethiopia ‘yazuia mashambulizi ya wanamgambo 450 wa Al-Shabaab’

0

Ethiopia imepuuzilia mbali video ya mtandaoni iliyotolewa na kundi la Al-Shabaab ambapo kundi hilo linasema lilishambulia msafara wa Ethiopia nchini Somalia na kuua wanajeshi 167.

Jeshi la Ethiopia lilitoa taarifa na kusema kuwa limezuia kabisa jaribio la shambulio lililofanywa Jumapili na wanamgambo 450 wa al-Shabab.

Kanali Feyisa Ayele, kamanda wa kikosi cha Ethiopia nchini Somalia, alisema al-Shabab pia wameacha magari matatu yaliyokuwa na vilipuzi kwenye barabara, ambayo wanajeshi wake waliharibu.

Hakutaja majeruhi yeyote wa Ethiopia katika taarifa yake.

Ni nadra kwa jeshi la Ethiopia kujibu ripoti za mashambulizi nchini Somalia, ambapo wanajeshi wake wanaunga mkono serikali katika azma yake ya kuwaangamiza wanamgambo wenye mafungamano na al-Qaeda.

Wakaazi wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mapigano hayo yalitokea karibu na mji wa kusini-magharibi wa Rab Dhure, karibu kilomita 20 (maili 12) kutoka mpaka wa Ethiopia.