Home Kimataifa Ethiopia kuwarejesha nyumbani raia 70,000 kutoka Saudi Arabia

Ethiopia kuwarejesha nyumbani raia 70,000 kutoka Saudi Arabia

0

Ethiopia imehiari kuwarejesha nyumbani raia wake 70,000 ambao wamekuwa wakiishi kwa hali duni nchini Saudi Arabia.

Shughuli hiyo itaanza rasmi mwezi Aprili. Yamkini raia hao wamekwama nchini Saudi Arabaia kwa muda mrefu na wanaishi katika mazingira duni, hali inayohatarisha maisha yao.

Ingawa kiwango cha pesa zitakazotumika kwa shughuli hiyo hakijatajwa, huenda mpango huo utaigharimu serikali kiasi kikubwa cha hela.

Ethiopia kwa sasa inatoa makao kwa wakimbizi 917,000 kutoka Sudan Kusini, Somalia, Yemen, Syria na Eritrea na wakimbizi milioni 4 wa ndani kwa ndani.

Website | + posts