Serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya hatari kufuatia kuenea kwa vita kati ya jeshi la kitaifa na wapiganaji kutoka kaskazini mwa eneo la Amhara.
Katika ujumbe wake kupitia mitandao ya kijamii, Waziri Mkuu Abiy Ahmed ametoa tangazo mapema Ijumaa ingawa hakutoa ufafanuzi endapo hali hiyo ya hatari ni ya nchi nzima au eneo la Amhara lililo kaskazini mwa mji mkuu wa Addis Ababa.
Vita vimechacha katika eneo la Amhara katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita na kusababisha serikali nyingi za kigeni kuwatahadharisha raia wake kuzuru Ethiopia au kuondoka wakati pia safari za usafiri wa ndege zikifutiliwa mbali.