Home Kimataifa Ethiopia yafanya mazungumzo ya ushirikiano wa kijeshi na Somaliland

Ethiopia yafanya mazungumzo ya ushirikiano wa kijeshi na Somaliland

Somalia inatafuta uungwaji mkono wa kimataifa kuhusiana na makubaliano tata ya Januari mosi kati ya Ethiopia na eneo la  Somaliland lililojitenga.

0

Ethiopia imesema imefanya mazungumzo Jumatatu kuhusu ushirikiano wa kijeshi na eneo lililojitenga la Somaliland.

Ushirikiano huo unajiri wiki moja tu baada ya makubaliano kati ya pande hizo mbili, kuhusu upatikanaji fursa ya baharini na kusababisha mivutano katika eno la uembe wa Afrika.

Mazungumzo hayo yaliyoandaliwa Jijini Addis Ababa, yalifanyika siku ambayo Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia alianza ziara katika nchi jirani ya Eritrea.

Somalia inatafuta uungwaji mkono wa kimataifa kuhusiana na makubaliano tata ya Januari mosi kati ya Ethiopia na eneo la  Somaliland lililojitenga.

Serikali kuu imeutaja mkataba huo wa maelewano (MOU),ambao unaipa Ethiopia fursa ya kuingia katika Bahari ya Sham kupitia Somaliland, kitendo cha ukandamizaji na ukiukaji wa uhuru wake.

Website | + posts
VOA
+ posts