Home AFCON 2023 Equitorial Guinea walenga ushindi katika derby ya Guinea AFCON

Equitorial Guinea walenga ushindi katika derby ya Guinea AFCON

0

Equitorial Guinea maarufu kama Nzalang Nacional ama radi ya taifa watashuka uwanja wa alasssane Ouattara mjini Abidjan Ivory Coast kwa mchuano wa tatu wa raundi ya 16 bora dhidi ya Guinea.

Nzalang Nacional watalenga kufuzu kwa kwota fainali kwa mara ya NNE baada ya kucheza raundi hadi raundi ya mwondoano katika makala yote manne waliyoshiriki mwaka 2012,2015 na 2021 .

Equitorial Guinea waliongoza kundi A kwa pointi 7 huku Guinea wakimaliza miongoni mwa timu bora za nafasi za tatu.

Guinea maarufu kama syli National wataazimia kutinga robo fainali kwa mara ya tano.

Timu zote zitakuwa zikikutana kwa mara ya kwanza katika awamu ya 16 bora.

Mchuano huo utango’a nanga saa mbili usiku majira ya Afrika Mashariki.