Home Biashara EPRA yaongeza bei ya bidhaa za mafuta

EPRA yaongeza bei ya bidhaa za mafuta

0

Halmashauri ya kudhibiti sekta ya kawi na mafuta nchini (EPRA), imetangaza bei mpya za mafuta kuanzia leo Jumamosi. 

Hii ni kufuatia kutiwa saini kwa mswada wa fedha wa mwaka 2023 kuwa sheria na Rais William Ruto.

Kufuatia kutangazwa kwa bei hizo mpya, bei ya lita moja ya mafuta aina ya Super itaongezwa kwa shilingi 13.49, Dieseli kwa shilingi 12.39 kwa kila lita na mafuta taa kwa shilingi 11.96 kwa kila lita.

Athari za kuongezwa kwa ushuru ziada wa thamani, VAT kwa bei za mafuta utahisiwa hata nje ya Nairobi, huku ukiathiri miji mikuu kote nchini Kenya.

Huku kiwango kipya cha VAT kikitekelezwa kuanzia leo bei ya mafuta ya super Mombasa sasa itakuwa shilingi 192.48 kwa kila lita, dieseli kwa shilingi 176.63 kwa lita na mafuta taa kwa shilingi 170.40 kwa lita.

Jijini  Nairobi, mafuta ya Super yatauzwa kwa shilingi 195.53 kwa lita, Dieseli kwa shilingi 179.67 kwa lita na mafuta taa kwa shilingi 173.44 kwa lita.

Hata hivyo bei hizo mpya huenda zisianze kutekelezwa jinsi ilivyopangwa kufuatia agizo la mahakama kuu lililositisha kwa muda utekelezaji wa sheria ya kifedha ya mwaka 2023 iliyofaa kuanza kutekelezwa tarehe mosi mwezi Julai mwaka huu.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here