Home Michezo Eliud Kipchoge kushiriki mbio za Marathoni za Berlin mwezi Septemba

Eliud Kipchoge kushiriki mbio za Marathoni za Berlin mwezi Septemba

Kipchoge alivunja rekodi yake ya dunia wakati aliposhinda mbio za marathoni za  Berlin Marathon kwa muda wa saa 2 dakika  01 na sekunde 09.

0
Eliud Kipchoge, anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za Marathoni.

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za marathoni Eliud Kipchoge atashiriki mbio za mwaka huu za marathoni za Berlin Septemba 24, akiwania ushindi wake wa tano.

Mwethiopia Tigist Assefa atatetea taji ya mbio za wanawake. Kipchoge alivunja rekodi yake ya dunia wakati aliposhinda mbio za marathoni za  Berlin Marathon kwa muda wa saa 2 dakika  01 na sekunde 09.

Kabla ya mbio hizo, Kipchoge alikuwa akijivunia ushindi wa mwaka  2015, 2017 na 2018. Kipchoge atakabiliana na mwenzake Amos Kipruto,  mshindi wa nishani ya shaba kwenye mashindano ya dunia mwaka 2019 na ambaye pia ni bingwa wa mbio za marathoni za London.

Katika kitengo cha wanawake, Tigist Assefa atakabiliana na Mkenya Sheila Chepkirui, mshindi wa nishani ya shaba kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola katika mbio za mita 10,000 na aliyemaliza wa nne kwenye mbio za marathoni za London mwezi Aprili kabla ya kuweka muda bora  wa saa 2 dakika 17 na sekunde 29, kwenye mbio za marathoni za Valencia mwezi Disemba.

Aidha, Chepkirui alishinda mbio za nusu marathoni za Berlin mwaka 2022 baada ya kuweka muda bora wa mbio hizo wa saa 1 dakika 05 na sekunde  02.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here