Home Kaunti Elijah Obebo aapishwa kuwa Naibu Gavana wa kaunti ya Kisii

Elijah Obebo aapishwa kuwa Naibu Gavana wa kaunti ya Kisii

0
kra

Elijah Obebo leo Jumatatu ameapishwa kuwa Naibu Gavana wa kaunti ya Kisii.

Hii inatamatisha uwezekano wowote wa kurejea kwa Naibu Gavana wa zamani Dkt. Robert Monda.

kra

Akiahidi kutimiza wajibu wake, Obebo alitaja uteuzi huo kuwa ishara kwamba watoto kutoka katika familia zisizojiweza, wanaweza kushika nyadhifa kuu katika jamii.

Awali, Wawakilishi Wadi 53 kati ya 70 walipiga kura ya kuondolewa kwa Dkt. Monda huku 15 wakipinga.

Bunge la Seneti baadaye lilikubaliana na mashtaka dhidi ya Dkt. Monda na kuthibitisha uamuzi wa kumwondoa afisini.

Maseneta 39 walipiga kura kuunga mkono mashtaka manne yakiwemo matumizi mabaya ya ofisi, kukiuka katiba na utovu wa nidhamu uliokithiri yaliyowasilishwa dhidi yake huku maseneta wanne wakipiga kura kupinga mashtaka hayo.

Obebo alimshukuru Gavana Simba Arati kwa kufikiria kumtwika wadhifa wa utawala wa kaunti.

Huku vijana wa Gen Z wakipanga kuandamana kesho Jumanne, Gavana Arati aliwasihi kuheshimu mali ya watu binafsi na ya umma watakapokuwa mitaani kesho na kusema uharibifu wowote utakuwa gharama kubwa siku zijazo.

Aliyekuwa jJaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Charles Nyachae alitoa changamoto kwa Arati na Obebo na kuonyesha uadilifu na utawala bora ambao wanahusishwa nao ikiwa kaunti hiyo itafanikiwa.

Obebo aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utumishi wa Umma ya kaunti hiyo.