Home Elaine Thompson-Herah afarakana na kocha wake

Elaine Thompson-Herah afarakana na kocha wake

Mshindi wa dhahabu tano za Olimpiki Elaine Thompson-Herah  amekatiza mkataba na kocha wake Shanikie Osbourne,kutokana na mzozo wa malipo, ikiwa mwaka mmoja kabla ya kutetea taji za mita 100 na 200 katika michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa.

Yamkini mwanariadha huyo aliye na umri wa mwaka 31, amelazimika kuchukua hatua hiyo, baada ya mazungumzo baina yake na kocha kuhusu malipo ya ridhaa aliyopaswa kumlipa.

Shirika linalosimamia mwanariadha huyo limetangaza kuanza mchakato wa kumtafuta kocha mpya kwa Elaine ambaye ameanza kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki.

Elaine aliandikisha historia kuwa mwanariadha wa kwanza wa kike kutwaa dhahabu za mita 100 na mita 200 katika michezo ya Olimpiki mwaka 2006 na 2001.