Home Burudani Eddie Kenzo atambulishwa nyumbani kwa wazazi wa mpenzi wake

Eddie Kenzo atambulishwa nyumbani kwa wazazi wa mpenzi wake

0
kra

Mwanamuziki tajika nchini Uganda Edrisa Musuuza maarufu kama “Eddy Kenzo” amethibitisha kwamba jana alitambulishwa nyumbani kwa wazazi wa mpenzi wake Phiona Nyamutoro, katika hafla ya kitamaduni ya ndoa.

Kenzo alichapisha picha za hafla hiyo mitandaoni na kuandika, “Sehemu ya kwanza imekamilika hivi karibuni mimi na marafiki tutarejea kumchukua mke.”

kra

Eddie na mpenzi wake Phiona ambaye ni mbunge anayewakilisha vijana katika bunge la Uganda wamechukua hatua ya kutambulisha na kuboresha uhusiano wao baada ya kuwa pamoja kwa miaka mingi kama marafiki.

Mwaka jana ndio walikiri kwamba wanapendana na sasa wameanzisha taratibu za kuoana kabisa.

Januari mwaka huu, Kenzo alisema kwenye mahojiano kwamba alikuwa tayari kuingia kwenye ndoa na ataandaa harusi kadhaa na mpenzi wake na wala sio moja.

Awali Kenzo alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki mwenza Rema Namakula na walibarikiwa na mtoto wa kike Disemba mwaka 2016 na ana binti mwingine na mwanamke mwingine.

Website | + posts