Home Taifa EACC yarejesha ardhi ya milioni 110 iliyonyakuliwa Nyahururu

EACC yarejesha ardhi ya milioni 110 iliyonyakuliwa Nyahururu

0
kra

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisad nchini, EACC imeirejeshea serikali ya kaunti ya Laikipia kipande cha ardhi cha ekari 2.5 ambacho thamani yake inakadiriwa kuwa milioni 110. 

Kipande hicho kilikuwa kimenyakuliwa na watu binafsi wapatao 12 mjini Nyahururu.

kra

Kulingana na EACC, ardhi hiyo ilikuwa imetengwa kwa ajili ya maegesho ya magari ya Nyahururu na kilikuwa kimenyakuliwa na watu binafsi kinyume cha sheria. Sasa kimerejeshewa serikali ya kaunti ya  Laikipia ambayo ni mmiliki wake halisi.

Msemaji wa EACC Eric Ngumbi anasema ardhi hiyo ilinyakuliwa na watu binafsi kinyume cha sheria na walikuwa tayari wameanza ujenzi wa majengo makubwa ya kibiashara EACC ilipoingilia kati.

Ngumbi aliyewahutubia wanahabari wakati wa ukabidhi wa ardhi hiyo mjini Nyahururu alisema EACC kupitia kwa Ofisi yake ya Kikanda ya Eneo la Kati iliyopo mjini Nyeri ilianzisha uchunguzi punde baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wa nguo za mitumba Februari 21, 2022.

Wafanyabiashara hao waliokuwa wakitumia ardhi hiyo kuendesha shughuli zao wakati huo walisema ardhi hiyo iliyokusudiwa kutumiwa kwa upanuzi wa maegesho ya magari ya Nyahururu ilikuwa imenyakuliwa na watu binafsi kinyume cha sheria.

 

 

Lydia Mwangi
+ posts