Home Kimataifa EACC yaonya dhidi ya ufisadi kwenye manunuzi ya El Nino

EACC yaonya dhidi ya ufisadi kwenye manunuzi ya El Nino

0
Bw. Twalib Mbarak
kra

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini, EACC imeonya dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma kwenye manunuzi yote yanayohusiana na maandalizi ya kushughulikia dharura ambazo huenda zikatokea wakati wa mvua inayotarajiwa ya El Nino.

Kwenye taarifa kwa maafisa wote wa manunuzi katika wizara na idara za serikali katika serikali kuu na serikali za kaunti, Mkurugenzi Mtendaji wa EACC Twalib Mbarak alisema wamefahamishwa kuhusu kutozingatiwa kwa sheria za manunuzi wakati wa kuanzisha na kutekeleza mipango ya kukinga umma kutokana na madhara ya mvua ya El Nino.

kra

Mbarak alihimiza maafisa hao kuzingatia sheria za manunuzi na sheria za usimamizi wa pesa za umma.

Ameonya kwamba kila mmoja atawajibika kivyake iwapo kutatokea hasara, matumizi yasiyoidhinishwa ya fedha na matumizi mabaya ya pesa za umma.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa ilitoa tahadhari ya uwezekano wa mvua ya El Nino kati ya mwezi Septemba mwaka huu na Januari mwaka ujao.

Kutokana na hilo, wizara na idara husika za serikali zimekuwa zikitekeleza mipango ya kukinga wananchi dhidi ya hatari ambazo huenda zikatokana na mvua hiyo kama vile mafuriko.

Website | + posts