Home Kaunti EACC yashikilia mali ya maafisa wa serikali ya kaunti ya Vihiga

EACC yashikilia mali ya maafisa wa serikali ya kaunti ya Vihiga

0

Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC), imepata maagizo ya mahakama ya kushikilia majengo mawili yaliyonunuliwa kwa kutumia fedha zilizoporwa kutoka serikali ya kaunti ya Vihiga.

Washukiwa wakuu katika sakata hiyo ni pamoja na mkuu wa kitengo cha ununuzi wa kaunti hiyo, wake zake wawili ambapo mmoja wao ni mfanyakazi wa kaunti hiyo, aliyekuwa afisa mkuu na mke wake, wote ambao ni wafanyakazi wa kaunti hiyo na watu wengine wanane.

EACC ilipata maagizo hayo jana Jumanne kupitia ombi la dharura katika mahaka kuu.

Majengo hayo yapo katika eneo la Nextgen Park makutano ya  Fourways, na thamani yake ni shilingi milioni 14 na milioni 13.5 mtawalia.

EACC imesema itatoa taarifa kamili kuhusu jinsi fedha hizo zilivyoporwa na washukiwa hao.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here