Home Habari Kuu EAC kutotekeleza uangalizi wa uchaguzi DRC

EAC kutotekeleza uangalizi wa uchaguzi DRC

0

Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC imesema kwamba haitatuma wawakilishi wake kutekeleza uangalizi wa uchaguzi mkuu nchini DR Congo kama ilivyo ada.

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha inaelezea kwamba Jumuiya hiyo haijapatiwa idhini inayohitajika kutoka kwa mamlaka husika ili kutuma waangalizi wa uchaguzi.

Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unairuhusu kutuma waangalizi wa uchaguzi kwenye nchi wanachama kwa mwaliko wa nchi husika.

Jumuiya hiyo inaitakia serikali ya DR Congo na watu wake uchaguzi wa amani ikisisitiza kujitolea kwake kuhudumia nchi zote wanachama .

Uchaguzi mkuu utaandaliwa kesho Jumatano Disemba 20, 2023 nchini Congo.

Website | + posts