Kwenye taarifa ya maandishi, Biden alisema kuwa marekani itachukua hatua kuwasaka wale waliotekeleza shambulizi hilo itakapoamua kufanya hivyo.
Mshirikishi wa mawasiliano katika baraza la kitaifa la usalama nchini marekani, John Kirby alisema kuwa marekani itachukua hatua kufuatia shambulizi hilo ila itasubiri uamuzi wa rais.
Matamshi yake yalikaririwa na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Antony Blinken aliyesema kuwa wanataka kuzuia mzozo huo kukithiri ila ni sharti walinde raia dhidi ya mashambulizi na wakati huo huo kuepusha mzozo.