Home Kimataifa Duale: Serikali itakabiliana na ukataji haramu wa miti

Duale: Serikali itakabiliana na ukataji haramu wa miti

Waziri huyo alisema ukiukaji wa sheria za misitu unahujumu juhudi za Kenya za uhifadhi wa mazingira.

0
Waziri wa Mazingira Aden Duale.
kra

Waziri wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi Aden Duale, ameahizi kumaliza ukataji haramu wa miti, katika misitu ya serikali.

Waziri huyo alisema ukiukaji wa sheria za utunzaji wa misitu unahujumu juhudi za Kenya za uhifadhi wa mazingira, zinazojumuisha ajenda ya serikali ya Kenya Kwanza ya upanzi wa miti bilioni 15.

kra

“Ukataji haramu wa miti, ujenzi wa makazi katika misitu, zimedumaza juhudi za uhifadhi wa mazingira, na kuhatarisha sio tu mazingira lakini pia mustakabali wa taifa hili,” alisema Duale.

Akizungumza leo Ijumaa katika sherehe ya 47 ya mahafali wa taasisi ya misitu ya Londiani katika kaunti ya Kericho, ambapo wanafunzi 197 walifuzu, Duale aliwaagiza maafisa wa huduma za misitu nchini kutekeleza kikamilifu sheria za kulinda misitu.

Wakati huo huo waziri huyo alitoa wito kwa wakenya kushiriki kikamilifu katika upanzi wa miti biliobi 15, akisema zoezi hilo litafanikisha juhudi za kukailiana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupiga jeki mipango ya kuimarisha maisha..

“Pamoja tunalenga kupanda miti bilioni 15, katika muda wa miaka kumi ijayo. Hili ni jukumu la pamoja, na ninatoa wito kwa kila mmoja kushiriki,” aliongeza Duale.

Website | + posts