Waziri wa Mazingira Aden Duale ataongoza sherehe za kuadhimisha sikukuu ya mazingira kesho Alhamisi.
Sherehe hizo zitafanyika katika bustani ya Arboretum, kaunti ya Nairobi.
Sherehe hizo zitaanza majira ya saa moja asubuhi na pia zitaadhimishwa katika kaunti zote 47 nchini.
Oktoba 10 imekuwa ikiadhimishwa kama sikukuu ya Moi lakini ikabadilishwa jina na kuitwa siku ya mazingira.
Duale amewarai Wakenya kutumia siku hiyo kutunza mazingira kupitia upanzi wa miti na uzoaji taka.