Home Taifa Duale azindua ujenzi wa nyumba za wanajeshi Laikipia

Duale azindua ujenzi wa nyumba za wanajeshi Laikipia

0
kra

Waziri wa ulinzi Aden Duale leo aliongoza uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa wanajeshi wa KDF katika eneo la Kwa Mbuzi, kaunti ya Laikipia.

Kulingana na waziri huyo, mradi huo wa nyumba 788 za makazi ni sehemu ya mpango mwingine mkubwa unaolenga kushughulikia suala la ukosefu wa nyumba za makazi kwa wanajeshi wa KDF nchini.

kra

Duale alifafanua kwamba kwa sasa KDF ina nakisi ya nyumba 33,400 kwa walio na familia na nakisi nyingine ya nyumba 25,800 kwa wanajeshi ambao hawana familia.

Chini ya mpango mpana wa kuongeza makazi ya KDF nchini, Duale alisema kwamba nyumba 3,069 zitajengwa katika maeneo matano humu nchini ikikumbukwa kwamba mwezi jana, alizindua ujenzi wa nyumba za KDF 952 katika kaunti ya Nakuru.

Huko Laikipia nyumba zitakazojengwa ni 788, 697 zinajengwa huko Gilgil, 120 huko Mariakani na nyumba 500 zitajengwa katika kaunti ya Nairobi.

Miradi hii ya nyumba za wanajeshi inafanikishwa na ushirikiano kati ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuhakikisha makazi bora kwa wanajeshi.

Duale alisema kwamba serikali imejitolea kutoa makazi ya ubora wa hali ya juu na endelevu kwa wanajeshi wake ili kuhakikisha mazingira bora ya kutekeleza kazi zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here