Droo ya awamu ya makundi ya kipute cha Ligi ya Mabingwa Afrika iliandaliwa Ijumaa, mechi hizo zikitarajiwa kusakatwa kati ya Novemba 24 mwaka huu na Machi 2 mwaka ujao.
Mabingwa wa mwaka 2016 Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini walijumuishwa kundi A pamoja na Pyramids FC kutoka Misri, Mabingwa wa mwaka 2015 TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na FC Nouadhibou kutoka Mauritania.
Wydad Casablanca ya Morocco waliocheza hadi fainali ya mwaka jana wamejumuishwa kundi B pamoja na Simba SC ya Tanzania, Asec Mimosas ya Cote d’Ivoire na Jwaneng Galaxy kutoka Botswana.
Esperance kutoka Tunisia wamo kundi C pamoja na have Atletico Petroleos ya Angola, Al Hilal ya Sudan na Etoile du Sahel ya Tunisia.
Mabingwa watetezi Al Ahly SC ya Misri wako kundi D pamoja na CR Belouizdad ya Algeria, Yanga ya Tanzania na Medeama kutoka Ghana.