Droo ya mechi za mchujo kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 kwa mataifa ya Afrika itaandaliwa Alhamisi, Julai 13 mjini Abidjan nchini Ivory Coast.
Shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF litaandaa droo hiyo sambamba na kikao cha kawaida cha 45.
Mataifa ya Afrika yatagawanywa katika makundi 9 huku mshindi wa kila kundi akijikatia tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2026 katika mataifa ya Marekani, Mexico na Canada.
Timu nne bora za nafasi ya pili kutoka makundi yote 9 zitafuzu kwa mchujo ambao baadaye, mshindi mmoja atajikatia tiketi kwa kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia.