Home Michezo Droo ya kufuzu AFCON 2025 kuandaliwa Alhamisi

Droo ya kufuzu AFCON 2025 kuandaliwa Alhamisi

0
kra

Droo ya fainali za mwaka 2025 kuwania kombe la mataifa ya Afrika itaandaliwa Alhamisi jioni nchini Afrika Kusini.

Mataifa 48 yatajumuishwa kwenye droo hiyo kila kundi likiwa na timu 4.

kra

Michuano ya kufuzu itaanza Septemba mwaka huu, huku timu mbili bora kutoka kila kundi zikifuzu kwa fainali hizo.

Makala ya 35 ya kindumbwendumbwe cha AFCON yataandaliwa katika viwanja sita vya miji sita nchini Morocco, kati ya Disemba 21 mwaka ujao na Januari 18 mwaka 2026.