Jamhuri ya Kidemokraisa ya Congo imeripoti vifo 35 vipya vya ugonjwa wa Mpox, na kufikisha idadi ya waliofariki tangu Januari mwaka huu kuwa zaidi ya 600.
Ripoti ya afya iliyotolewa jana na Wizara ya afya nchini humo imeashiria kuwa ugonjwa huo umeripotiwa katika kila pembe ya nchi hiyo, na kuifanya kuwa taifa lenye maambukizi ya juu zaidi Afrika.
Waziri wa afya ya umma Dkt Dr Roger Kamba,alisema kuwa kuliripotiwa na visa 1,372 vipya vinavyoshukiwa ,maambukizi 206 mapya na vifo 35.
Kamba amesema jumla ya watu 17,801 wameambukizwa ugonjwa huo tangu Januari mwaka huu, huku mikoa yote 26 ikiwa imeathiriwa.