Home Habari Kuu Dorcas: Wakumbatieni walio na matatizo ya afya ya akili

Dorcas: Wakumbatieni walio na matatizo ya afya ya akili

Dorcas alihimiza jamii kuwakumbatia wanaoathirika na afya ya akili.

0
Mchungaji Dorcas Rigathi.

Mke wa naibu rais mchungaji Dorcas Rigathi, ametoa wito kwa wakenya kuwasaidia wale walio na changamoto ya afya ya akili, kukabiliana na hali hiyo.

Akizungumza alipofungua kongamano kuhusu afya ya akili katika chuo kikuu cha Daystar, Dorcas alihimiza jamii kuwakumbatia wanaoathirika na afya ya akili.

“Hata katika hali hiyo, ikiwa utakuwa na familia inayokusaidia na jamii ambayo inakuelewa, ni rahisi kukabiliana na hali hiyo na pia kuwasaidia wengine,”alisema Dorcas.

“Ikiwa jamii inayokuzingira haikuelewi wala kukusaidia, basi hali hiyo itakuthuru zaidi na hata kusababisha maafa. Afya ya akili ni janga katika taifa hili na dunia nzima kwa jumla, hata katika vyuo vikuu,”aliongeza mchungaji Dorcas.

Afisa mkuu mtendaji wa My Afya Africa, aliunga mkono matamshi ya mchungaji Dorcas, akiongeza kuwa afya ya akili ni jukumu la jamii.

“Afya ya akili sio swala la mtu binafsi, lakini ni jukumu la jamii. Mmoja wetu hajaathirika, nina hakika tumekumbana na swala hilo,”alisema afisa huyo.

Mkutano huo huwaleta pamoja wanafunzi wa vyuo vikuu, vyuo anuwai, taasisi za kiufundi na washika dau wengine.

Website | + posts