Ipo haja ya kuwawezesha wajanae kiuchumi hapa nchini, ili wajimudu pamoja na familia zao, haya ni kwa mujibu wa mkewe wa naibu Rais Dorcas Rigathi.
Dorcas alidokeza kuwa taifa hili lina zaidi ya wajane milioni nane, na wengi wao wanahangaika kushughulikia familia zao baada ya waume wao kuaga dunia.
Akizungumza akiwa Kimana, Kajiado kusini, kaunti ya Kajiado alipozindua chama cha akiba na mikopo cha wajane wa Loitokitok, Dorcas alisema wajanane hukumbwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na kutengwa, kubaguliwa, ukosefu wa fedha, changamoto za kimawazo na hivyo kuwa vigumu kwao kushughulikia familia zao.
“Wajanae hukumbana na changamoto nyingi katika jamii, na ni sharti wawezeshwe kiuchumi ili nao pia waishi maisha ya heshima na kukimu mahitaji ya familia zao,” alisema Mchungaji Dorcas.
Aliongeza kuwa kwa muda wa miaka mingi, wajane wametengwa na hawajakuwa wakipata huduma za fedha, hali iliyosababisha kubuniwa kwa chama cha akiba na mikopo kuwawezesha kuwekeza na pia kuchukua mikopo.
“Uzinduzi wa chama hichi cha akiba na mikopo, utawawezesha kupata mikopo ya riba nafuu, kushughulikia mahitaji yao na pia watapa mafunzo kuhusu fedha ili kuimarisha biashara zao,” aliongeza Dorcas.